TCRA LOGO VIDOLE

Featured Posts

Friday, November 21, 2014

WABUNGE WARUKA UKUTA KUINGIA BUNGENI...


Ukweli ni kwamba kuna story ambayo unaweza ukasimuliwa na rafiki yako ama mtu yoyote halafu ukaona kama ni uzushi na hakuna ukweli wowote.
Pata picha pale ambapo Spika wa Bunge pamoja na Wabunge wanafungiwa geti la kuingia ndani ya Ukumbi Bunge …
Nakupa story kutoka Nigeria, Spika wa Bunge la Nchi hiyo Aminu Tambuwal amelazimika kuingia ndani ya Bunge kupitia mlango mdogo wa dharura baada ya Polisi kufunga milango ya Bunge hilo kwa sababu za kiusalama.

MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO MJINI AENDELEA KUTEKELEZA ILANI YA CCM


 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood akiongea ofisini kwake wakati akikabidhi Vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Jimbo la Morogoro Mjini Ikiwa ni Utekelezaji wa Ahadi zake alizotoa Kipindi Akiomba kura ya Kuwa Mbunge wa Jimbo Hilo Pamoja za Ahadi anazotoa kwenye Mfululizo wa Ziara zake anazofanya Mara kwa mara katika Kata Mbalimbali za Jimbo la Morogoro Mjini.
 Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Azizi Abood akikabidhi Mboa kwa Viongozi wa Msikiti kwajili ya Kumalizia ujenzi wa Msikiti ikiwa ni ahadi aliyoitoa wakati wa ziara zake za mara kwa mara.

LETS ALL SUPPORT MISS TANZANIA AT MISS WORLD 2O14

MAGAZETI YA LEO IJUMAA TAREHE 21.11.214

.

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.

MAGAZETI YA UDAKU LEO

.

Polisi wakiwaokoa wachezaji Ivory Coast Baada Ya kuvamia Uwanjani

Kufuzu kwa Ivory Coast kucheza fainali za Africa mwakani kumegubikwa na tukio la mashabiki wa nchini humo kuvamia uwanja kwa furaha baada ya kumalizika mchezo huo dhidi ya Cameroon uliomalizika kwa sare 0-0 huko Abidjan.WATU WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MBEYA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 20.11.2014.
  • WATU WAWILI WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI.JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA NYAKATI TOFAUTI WAKIWA NA BHANGI PAMOJA NA MICHE YA BHANGI. KATIKA MSAKO WA KWANZA, MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KATSON IYISEGA (68) MKAZI WA KIJIJI CHA ISWAGO ALIKAMATWA AKIWA AMEOTESHA MICHE YA BHANGI 12 KATIKA SHAMBA LAKE LA MAHINDI. MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 19.11.2014 MAJIRA YA SAA 11:30 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISWAGO, KATA YA SANTILYA, TARAFA YA ISANGATI, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI WA BHANGI NA TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAENDELEA.

WAZIRI MKUU PINDA AKIWA BUNGENI MJINI DODOMA

Waziri Mkuu,Mizengo Pinda  akiteta na Mbunge wa Urambo na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta, Bungeni Mjini Dodoma Novemba 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MHE. MOHAMED CHANDE OTHMAN, JAJI MKUU WA TANZANIA ATEMBELEA UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, WASHINGTON DC 19/11/2014


Mhe. Mohamed Chande, Jaji Mkuu wa Tanzania akisaini kitabu cha wageni katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Washington DC, Marekani.

Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania (Wa Tatu Kushoto)katika picha ya pamoja na Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC na watumishi wengine wakati wa ziara yake Ubalozini. Wa nne Kushoto, ni Mhe. Prof. Ibarahim Juma, Jaji wa Mahakama ya Rufaa na wa Pili kulia ni Mhe. Aloysius Mujulizi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

KINANA ATAKA UTARATIBU WA AJIRA SERIKALINI UANGALIWE UPYA

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa kuna haja ya kubadilisha taratibu za ajira badala ya kuwa za kudumu ziwe za mikataba kwani itasaidia kufanya kazi kwa ufanisi.

WABUNGE WACHARUKA KASHFA AKAUNTI YA TEGETA-ESCROW NI SHEEEEDA

Naibu spika wa bunge Job Dungai, yeye ndiye kashikilia rungu, Ripoti " ijadiliwe au la"
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), Ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali, (PAC), Zitto Kabwe. Taarifa ya CAG kuhusu akaunti nya Tegeta Escrow, iko mikononi mwake

Thursday, November 20, 2014

LORI LALIPUKA ENEO LA MIKUMI MKOANI MOROGORO

 Tumepokea picha ya tukio la ajali ya Lori lililokuwa limebeba mapipa ya lami ambalo limeshika moto mapema leo asubuhi maeneo ya Mikumi, Morogoro.chanzo cha mlipuko huo bado hakijafahamika mpaka sasa na bado hatujapata taarifa kama kuna aliepoteza maisha au kupatwa kwa majeruhi.Chini ni ujumbe kutoka kwa mdau wetu  alietuletea taswira hizi kuhusiana na hali ya barabara hiyo.

ANGALIA VIDEO MPYA KALI: DIAMOND PLATINUMZ - NITAMPATA WAPI..

MAALIM SEIF ATEMBELEA ENEO LA JENGO LILILOANGUKA JANA MJI MKONGWE ZANZIBAR


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad akimsikiliza Kamanda Ame Ali ambaye ni kiongozi wa shughuli za usafishaji wa eneo lilipoanguka jengo la ghorofa huko Shangani mjini Zanzibar.

MUNGU WANGU! MAMA AJIFUNGUA MTOTO WA AJABU DAR!

My God! Mama aliyetambulika kwa jina la Swaumu Sadick (25), mkazi wa Manzese jijini Dar, amejikuta yeye na manesi wakitimua mbio kwa woga baada ya kujifungua kiumbe wa ajabu.

Swaumu Sadick akiwa hospitali baada ya kujifungua mtoto huyo. Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo ambalo kwa sasa ni gumzo, lilijiri hivi karibuni mishale ya saa 8:00 usiku kwenye Kituo cha Afya Cha Kijiji cha Mlali kilichopo wilayani Mvomero mkoani hapa.

MAGAZETI YA LEO ALHAMISI TAREHE 2O.11.2O14

.

MAGAZETI YA UDAKU LEO


MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI

.

BREAKING NEWSS : LORI LINATEKETEA KWA MOTO MUDA HUU

 Lori lilokuwa limebeba shehena ya Mapipa ya Lami ikiteketea kwa Moto muda huu eneo la Mikumi Mkoani Morogoro Barabara kuu ya Morogoro Iringa

GHANA YAAMKA, YAICHAPA TOGO YA ADEBAYOR 3-1, YAFUZU AFCON

Pamoja na kucheza bila Gyan Asamoh na Andre Ayew Ghana imefanikiwa kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (Afcon).
Black Star imefanikiwa kufuzu kwa kuichapa Togo iliyoongozwa na Emmanuel Adebayor iliyokuwa ugenini kwa mabao 3-1, leo.
Kutokana na ushindi huo, Ghana imefikisha pointi 11 na kufuzu katika michuano hiyo mikubwa ya soka Afrika kwa timiu za taifa.
Ghana ilionekana kuizidia Togo kwa kila kitu huku safu ya ushambuliaji ya Ghana ikiichachafya safu ya ulinzi ya wageni.

WATOTO 130000 WANAISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

unnamed
Wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi waliohudhuria kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ufunguzi wa kongamano hilo. Hadi sasa watoto wenye maambukizi ya VVU 130000 wameweza kufikiwa kati ya hao 39317 wamepewa dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo.
Picha na Anna Nkinda – Maelezo
unnamed1
Baadhi ya wajumbe kutoka asasi za umma na za binafsi za ndani na nje ya nchi zinazoshughulikia mambo ya Ukimwi wakimsikiliza Naibu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Dkt. Pindi Chana (hayupo pichani) wakati akifungua kongamano la nne la kitaifa linalohusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi kwa watoto. Kongamano hilo la siku mbili limeandaliwa na Taasisi ya Elizabeth Glaser Pediatric Aids (EGPAF).

TTCL YAKABIDHI MSAADA WA MABENCHI KATIKA KITUO CHA AFYA BUGURUNI

unnamed2Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho Dtk. Mwajuma Mbaga akiishukuru TTCL kwa msaada walioutoa na kuwaomba wadau wengine wasaidie kituo hicho kwani  kinahudumia wagonjwa zaidi ya 350 kwa siku
unnamedWafanyakazi wa kituo hicho katika picha ya pamoja.

KINANA ASHIRIKI KILIMO KATIKA SHAMBA LA UFUTA LA KIKUNDI CHA (UMOJA RIKA) KATIKA KIJIJI CHA MKOTOKUYANA NACHINGWEA

1Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh.  Mathias Chikawe wakati alipowasili katika kijiji cha Mkotokuyana jimbo la Nachingwea katika mwendelezo wa ziara yake ya mikoa ya Lindi na Mtwara itakayomchukua siku 16 akikagua utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa  na srikali kwa pamoja na wananchi huku akihimiza uhai wa Chama cha Mapinduzi katika vijiji mbalimbali , Majimbo na wilaya Katika ziara hiyo Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi. (PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-NACHINGWEA-LINDI)3Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi akizungumza na  Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya msafara wa Katibu Mkuu kuwasili katika kijiji cha Mkotokuyana4Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliiza Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mhe. Regina Chonjo mara baada ya kufika kwenye shamba la ufuta la Kikundi cha Umoja Rika  leo kijijini hapo, Kulia ni Mbunge wa jimbo la Nachingwea Mh. Mathias Chikawe na kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa, Itikadi na Uenezi

WATATU WAKAMATWA NA DOLA FEKI ZENYE THAMANI YA MILIONI 20

Dola bandia

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Fresser Kashai akiwaonyesha waandishi wa habari mkoani hapa Dola Feki za kimarekani. Picha na Elizabeth Kilindi, Tanga.

TAMISEMI YATANGAZA TAREHE YA KUJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

 Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Bwn. Khalist Luanda akizungumuza na waandishi habari juu ya kukamilika kwa maandalizi ua uchaguzi wa Serikali za Mitaa miji Dodoma leo. Bwn. Khalist Luanda alitangaza rasmi tarehe ya kujiandikisha na kupiga kura.(Picha na habari kutoka Oya Waziri Mkuu TAMISEMI)
Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa Bwana Kharist Michael Luanda amesema wananchi wanapaswa kujiandikisha katika daftari maalum la kupigia kura kwa ajili ya kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kuanzia tarehe 23/11/2014 hadi tarehe 29/11/2014. 
Mkurugenzi huyo alisema kuwa wananchi wanaotaka kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi za vijiji, vitongoji na mitaa wanapaswa kuchukua fomu za kugombea kuanzia tarehe 16/11/2014 hadi tarehe 22/11/2014. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, Bwana Luanda aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha ili waweze kupata fursa ya kushiriki katika kupiga kura ili kuwachagua viongozi wa vijiji, vitongoji na mitaa wanaowataka.
Alisema sifa za mtu anayestahili kujiandikisha kushiriki uchaguzi huo ni lazima awe raia wa Tanzania, mwenye umri wa miaka 18 au zaidi, mkazi wa eneo hilo na mwenye akili timamu.

CHINGAS WALIVYOPAMBANA NA POLISI JIJINI MWANZA

Polisi wa kutuliza ghasia, wakifanya doria kwenye mitaa ya jiji la Mwanza baada ya kutokea ghasia kufuatia askari wa jiji hilo kufanya jaribio la kuwaondoa wamachinga kwenye soko kuu, rwagasore na mtaa wa Lumumba mapema leo Jumatano Novemba 19, 2014

WANAFUNZI ST.JOHNS DODOMA WAGOMA MPAKA KIELEWEKE

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo kikuu cha St Johns Manispaa ya Dodoma Danny Damian akiwahutubia wenzake, kwenye uwanja wa michezo wa Chuo hicho leo Jumatano Novemba 19, 2014. Wanafunzi hao wametangaza mgomo wa kutoingia madarasani hadi hapo kero zao zote zitakaposhughulikiwa na uongozi, kubwa kuliko zote ni uhaba wa walimu na hata wale waliopo uwezo wao wa kufundisha haukidhi viwango. Wanafunzi hao wameenda mbali zaidi na kuutaka uongozi wa chuo hicho kilicho chini ya kanisa moja hapa nchini, kukirudisha serikalini kama "Ngoma" imewashinda

SNOW ILIYOANGUKA BAFFALO, NEW YORK, WATANO WAPOTEZA MAISHA

Theluji iliyoanguka siku ya Jumanne kuamkia Jumatano mji wa Baffalo jimbo la New York theluji iliyokanguka ilifikia futi 5 imesababisha vifo vya watu watano, wawili kati yao wamepoteza maisha kutokana na ajali za magari yao kuseleleka na wengine watatu wamekufa kutokana heart Attack. Pichani ni mkaazi wa Baffalo akijaribu kuparua theluji hiyo kabla haijaganda na kuwa barafu.

BINTI AJINASUA NA NDOA YA MWANAMGAMBO WA IS


Raia wengi kutoka Ulaya wamejiunga na kundi la wapiganaji wa Islamic State nchini Syria
Mwanamke mmoja raia wa Uholanzi amewasili nchini Uturuki baada ya safari iliyojaa hatari nchini Syria kwa ajili ya kumchukua binti yake aliyekua mjini Raqqa, mji unaokaliwa na waasi wa Islamic State.Monique alikwenda Uturuki mara ya kwanza baada ya binti yake aitwae Aicha kusafiri kwenda Syria kuoana na mmoja wa wanamgambo wa kundi hilo mwenye asili ya Uholanzi na Uturuki.Mamia ya Wanamgambo wenye asili ya Ulaya wamekua wakienda Syria kupigana ndani ya kundi la IS.Aicha ,19 ni miongoni mwa Wasichana ambao walisafiri kujiunga na IS.Raia wawili wa Austria wenye umri wa miaka 15 na 17 walikwenda Syria Mwezi Aprili na mmoja wao aliripotiwa kuuawa.Aicha aliondoka Uholanzi mwezi Februari, akaolewa na Omar Yilmaz, mwanamgambo mwenye asili ya Uturuki na Uholanzi ambaye alishawahi kuwa mwanajeshi nchini Uholanzi,alitumia mbinu alizopatiwa akiwa mwanajeshi na kuwafunza wapiganaji wenzake.

Wednesday, November 19, 2014

MWANAFUNZI BORA UDSM.. NILIMPA MOTISHA YAKE 2011 NA SASA KAWA BORA ZAIDI..MEYA JERRY SILAA


Doreen Kabuche akiwa na Meya wa manispaa ya Ilala Mhe.Jerry Sila jijini Dar es Salaam Leo alipoenda kupongezwa kwa kuwa mwanafunzi bora aliyehitimu Chuo kikuu cha Dar es Salaam mwaka huu..

BILIONEA WA DUNIA BILL GATES KUSAIDIA KUPAMBANA NA EBOLA

Bill Gates na Melinda Gates.
MFUKO wa Bill na Melinda Gates umeahidi kutoa kiasi cha dola milioni 5.7 kwa ajili ya mradi kusaidia matibabu dhidi ya maradhi ya Ebola nchini Guinea na nchi nyingine zilizoathiriwa na ugonjwa huo.
Mfuko huo pia umesema msaada huo utasaidia kutathimini dawa za majaribio.
Zaidi ya Watu 5,000 wamepoteza maisha kutokana na Ebola, karibu wote kutoka Afrika Magharibi.

KANALI BIROCHO NZANZU AHUKUMIWA KIFO CONGO

Kanali Birocho Nzanzu
MAHAKAMA ya kijeshi Mashariki mwa Jamuhuri ya Demokrasi ya Congo imemhukumu kifo Kanali Birocho Nzanzu baada ya kubainika na makosa ya kutaka kumuua afisa wa jeshi la nchi hiyo.
Nzanzu anatuhumiwa kwa kosa la kutaka kumuuwa afisa aliyekuwa mstari wa mbele kutokomeza wapiganaji wa M23.
Afisa huyo anayedaiwa kupangiwa njama za kuuawa ni Mamadou Ndala ambaye kwa kiasi kikubwa aliamini katika vita dhidi ya kundi la wapiganaji wa M23 na  aliuawa mwezi Januari mwaka huu.

TRA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA KWA HOSPITALI YA MNAZI MMOJA,ZANZIBAR LEO.


Mkurugenzi wa Walipakodi na Elimu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Richard Kayombo (wa tatu kulia) akimkabidhi Mkurugenzi wa Idara ya Hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar,Dkt. Jamala Adam Taib (wa tatu kushoto) sehemu ya msaada wa vifaa tiba vya hospitali vilivyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania vyenye thamani ya shilingi Mil. 20 vitakavyotumiwa katika hospitali hiyo leo Novemba 19,2014,Zanzibar. 
Makabidhiani hayo yamefanyika kufuatia muendelezo wa Maadhimisho ya Wiki ya Mlipa Kodi Tanzania ya TRA yenye Kauli mbiu isemayo Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na Unapouza ni Lazima Utoe Risiti" .Wa pili ni Kaimu Kamishna wa TRA (Zanzibar),Mcha Hassan Mcha akiwa pamoja na maofisa wengine wa TRA.
 
 
Blogger Templates