TCRA LOGO VIDOLE

,.,.,

http://vbusiness.co.tz/

Monday, January 20, 2014

MIAKA 25 YA NDOA YA BETTY NA CHARLES MKWASA

Wana Silver Jubilee, Betty Mkwasa mabye ni Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma na mumewe Charles Boniface Mkwasa 'Master' Kocha msaidizi wa Yanga, wakionesha hati maalum ya ndoa kutoka kwa Papa Francis. Hati hiyo ya heshima hutolewa na Papa kwa wanandoa waliotimiza miaka 25 ya ndoa yao. Mkwasa na mkewe walitimiza miaka 25 ya ndoa yao Januari 14 mwaka huu na jana Januari 18 kuafanya misa maalum ya kubariki ndoa yao na kurejea viapo vyao vya ndoa. 
Haya ndio matunda ya ndoa ya Bwana na Bibi Mkwasa
 Waziri wanchi ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge, Willium Lukuvi na mkewe nao walikuwepo. Katkati ni Mama mzazi wa Betty Mkwasa.
 Hawa vijana kushoto na kulia ndio walikuwa watoto waliokuwa wasindikizaji wa ndoa yao hivi sasa ni watu wazima. 

Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Dodoma wakiwa na wake zao wakipiga picha na maharusi. Wa tatu kulia ni Mbunge wa Bahi.
Wakulima na wananchi kutoka Bahi ambako Mheshimiwa Betty Mkwasa anafanyia kazi walileta kuku wa kienyeji na mafuta ya alizeti lita zaidi ya 30, Ng'ombe, Mbuzi, Kondoo, bata Mzinga na nafaka za mahindi na mchele kwa maharusi. 

No comments:

 
 
Blogger Templates